Lil Wayne akiwa na kitu chake kipya, Video Vixen Candance Cabrera.
New Orleans, Marekani. Rapa Lil wayne amemfungashia virago aliyekuwa laaziz wake wa zamani, Dhea na kuamua kuhamishia pendo lake kwa mwanamitindo na Video Vixen daraja la kwanza, Candance Cabrera ‘Black Flavor of love’ aliyekuwa mshiriki wa kipindi maarufu cha Flavor Of Love mwenye umbo la kuwatoa udenda wanaume wakware.
Awali Weezy aliwahi kuripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri na mpenzi wake wa zamani aliyekuwa mhudumu wa hoteli kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi baina yao huku kukiwepo kwa tetesi za chini kwa chini kwamba zilipendwa huyo aliwahi kufumwa nyumbani kwa Drake wakiwa wawili jambo ambalo liliibua mzozo baina ya wakali hao.
Pichani ni Mrembo Candace Cabrera.
Lil Wayne akiwa na zilipendwa wake aliyempiga kibuti, Dhea enzi za penzi lao.
Post a Comment