Hivi ndivyo alivyosimulia kwenye kipindi cha Mkasi cha wiki iliyopita:
“Tulikuwa muda mrefu sisi tunadate muda mrefu, mimi baadaye nikamchana ‘ooyah mimi nataka tuoane’ kipindi kile Vivica kashazaliwa ana kama miaka miwili mitatu akaniambia poa. Kwahiyo sisi tukaenda kanisani tukamkuta Padre tukamwambia ‘ooyah sisi tunataka kuoana,ikiwezekana hata leo’ Padre akatuambia ‘bwana nyie inabidi mfanye hata mafundisho tuwaelekeze ndoa ni nini’. Sasa mimi nikawa na kampeni muda,kila siku tuwe tunakuja tunafundishwa, akatuambia ‘naomba niwafundishe two weeks lakini kila Jumamosi’. Kwahiyo tukafundishwa kama Jumamosi hii na inayofuata, halafu inayofuata nikapiga tai yangu mimi na mnyamwezi wangu Steve B,mnyamwezi wangu Mark Dizzo tukaingia kanisani. Kwahiyo kanisani kulikuwa na kama watu sita likapigwa harusi moja hatari sana. Nilivyotoka baba akajoin, yaani baba amejua kwamba mimi naoa siku hiyo hiyo,aka join nini speech yake nakumbuka alisema ‘mimi sijui hata niseme nini maana umeniambia leo unaoa ,sina zawadi sijui nifanyeje’ Kwahiyo tukachill baadaYe ‘madingi’ wakaenda home na sisi tukaenda Bilicanas kula debe, wife na shela lake mimi na suti zangu,kwaHiyo ilikuwa hivyo.”
Post a Comment