Shirika la ndege la Malaysia Airlines limesema sasa linaweza kusema (beyond any reasonable doubt) kuwa ndege ya MH370 imepotea na hakuna manusura.
Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak amesema wachunguzi wa Uingereza wamedai kuwa eneo la mwisho ndege hiyo ilikuwa ni katikati ya bahari ya hindi magharibi mwa Perth.
Tangazo hilo limetolewa kwa ujumbe mfupi na imetumwa kwa familia ya abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo. Ndege hiyo iliyokuwa na watu 239 ilipotea March 8 na ilikuwa ikitokea Kuala Lumpur.
Shughuli za kutafuta mabaki ya ndege hiyo kwenye bahari ya Hindi imeingia siku ya tano.
Post a Comment