Mwanzo » » MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU APATIKANA AMEFARIKI NDANI YA DIMBWI LA KUOGELEA

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU APATIKANA AMEFARIKI NDANI YA DIMBWI LA KUOGELEA

Imewekwa ma Click BongoTz siku Tuesday, 25 March 2014 | 00:23

HALI ya taharuki inaendelea kutanda katika chuo kikuu cha Nairobi baada ya nwili wa mwanafunzi kupatikana ndani ya dimbwi la kuogelea la chuo hicho.


clip_image001

Mwili wa Mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kama Denis Maina, ulipatikana ndani ya dimbwi hilo ukiwa na nguo pamoja na viatu na kuzua wasiwasi iwapo aliuawa kwingine na mwili wake kutupwa hapo.
Wenzake ambao walikuwa wanatumia bwawa hilo walichukua saa mbili kutambua iwapo mwanafunzi huyo alikuwa amekufa.
“Denis alikuwa mwanafunzi wa masuala ya uchumi na alikuwa amebakisha mwezi mmoja kukamilisha masomo yake. Haikuwa rahisi kutambua mwili wake kwa sababu ya hali mbaya ya maji ya kuogelea,” alisema Joe Mugendi mwanufunzi wa chuo hicho.
“Wanafunzi walifunguliwa kutumia bwaha hilo saa nane jioni na saa mbili baadaye ndio mwili huo ulipatikana,” akasema.
Maafisa wa polisi waliondoa mwili wa mwanafunzi huyo na kufunga bwaha hilo ambalo hutumiwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Zack Kinuthia, Mwenyekiti wa Muungano wa wanafunzi katika chuo cha Nairobi (SONU) alitaka polisi ifanye uchunguzi wa haraka kubaini hali ambayo mwanafunzi huyo aliuawa.
“Tungependa polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili tujue ukweli,” alisema Bw Kinuthia.
Ukarabati
Wanafunzi wa chuo hicho walilalamikia utunzi mbaya wa bwaha hilo la kuogelea na kuitaka mamlaka ya chuo hicho kulisafisha na kukarabati majengo yake.

“Haifai kwa wanafunzi kuogelea kwa saa mbili ndani ya dimbwi lenye mwili wa mwenzao bila kuutambua, lazima mamlaka isafishe na kujenga upya bwawa hilo kwa sababu hatutaki matukio kama haya kushuhudiwa tena,” alisema Bw Mugenda.
Juhudi zaTaifa Leo kuwasiliana na mamlaka ya chuo hicho hazikufaulu kwani maafisa walidinda kuzungumzia kisa hicho hadi polisi wakamilishe uchunguzi wao.
Kisa hicho kimejiri wakati ambapo visa vya wanafunzi wa vyuo vikuu kuuawa vimekuwa vikiongezeka kwa kasi.
Aidha, sasa kuna hasira miongoni mwa wazazi kwamba hata watoto wao katika shule za upili wanafariki katika hali ya kutatanisha.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa