STUDIO YA RADIO YA KISASA. |
VIFUATAVYO NI VIPENGELE MUHIMU KATIKA KAZI HIYO.
1. MATUMIZI YA SAUTI.
Siku zote ifahamike kuwa utangazaji mtaji wa kwanza ni sauti na katika kuutumia mtaji huo kuna kila sababu ya mtangazaji kuitumia vizuri katika kuwapata mashabiki wanopenda matumizi yake ya sauti yaani sauti yako kama mtangazaji itumie ifuatavyo...
(a). Epuka kuigiza sauti-Maana ya hoja hii ni kwamba unapokuwa ukiongea katika microphone(Kipaza sauti) inakubidi uwe na mazungumzo kama unavyoweza kuwa ukizungumza na mtu katika maisha ya kwaida.
(b). Weka nafasi kimo cha kiganja chako kutoma microphone ilipo na mdomo wako na mazungumzo ya sauti yawe katika kiasi cha katikati yaani sauti isiyo ya juu wa isiyo ya chini.
(c). Katika kuongea kila mtu ameumbwa tofauti na kama wewe ni miongoni mwa waogeaji wale wanapokuwa wakiongea lazima watoe ushara za mikono na kusisitiza kwa vitendo itabidi uwe hivyo hivyo utakapokuwa ukizungumza katika microphone(Kipaza sauti).
(d). Ni muhimu unapokuwa ukiongea kama utakuwa na mtangazaji mwenzako msikilize huku ukimtazama usoni ili kwenda sawa na yeye kihisia na kimawazo ili wewe katika uchangiaji wa hoja anayoizungumzia kusiende nje ya leongo la mazungumzo.
2. MIKAO KATIKA STUDIO/HASA ZA RADIO.
Mara nyingi kuna vile mtu uwa huru katika mazungumzo yake na kuna mitindo tufauti ambayo watu uitumia ili kuwa huru katika mazungumzo.Kwamfano kuna watu anapokuwa akizungumza lazima atoe ishara za mikono na miguu hivyo watu hawa wa namna hii ni ngumu kuzungumza akiwa amekaa,wao inakuwa rahisi sana kuzungumza wakiwa wamesimamama.
Kuna watu wengine upenda kuzungumza wakiwa na hali flani ya kuinama na kuwekelea mikono muelekeo wa anayeongea nae na kama atakuwa pekee yake studio kwa upande wa radio atakuwa ameinamia uelekeo wa kipaza sauti(Microphone) na hii ni haina nyingine ya mikao huru kwa watangazaji kuzungumza na wasikilizaji.
Angalizo: Kama mtangazaji kaa mkao wowote ambao utakuwa ni rahisi kwako kuweza kuongea katika kipaza sauti.
3. KIJIAMINI.
Katika maongezi ya mtangazaji endapo mtu hautajiamini basi sauti yako itakuwa ikitoka ikiwa ni yaoga na isiyo na wasifu wa hali uliyonayo au unayoizungumzia. Mtangazaji unapokuwa na hali ya uogo pia unaweza kusahau kile unachokizungumzia na kwa wasikilizaji kuonekana kama haujui unazungumza nini na hata kama umeandika sehemu i rahisi katika usomaji ukachanganya mambo na ukasoma kwa kusita sita picha ambayo inakuwa sio nzuri kwa msikilizaji.
4. MAANDALIZI YA MAPEMA KABLA YA KUINGIA KATIKA KUZUNGUMZA KATIKA KIPAZA SAUTI(MICROPHONE)
Naamini inafahamika kuwa kila jambo linapokuwa namaandlizi mazuri siku zote linakuwa na asilimia kubwa ya kuenda vizuri na hapa katika utangazaji MAANDALIZI ni jambo muhimu la kuzingatia na hapa tnapozungumzia maandalizi hatumaanishi maandalizi tu bali tunamaanisha MAANDALIZI MAZURI hii inasisitizwa kujiandaa vizuri kwasababu wapo watangazaji wanojiandaa lakini sio kikamailifu jamabo ambalo akiwa katika utangazaji linaweza kuonesha kupwaya katika mazungunzo ingawa kuna watu wanaweza sigundue hilo ila kwa wenye uelewa na wengine hata wasio husika na utangazaji wanaweza kugundua uhafifu wa maadalizi ya mhusika.
Maadalizi bado yana misingi yake yaani hakikisha kile ulichokiandaa kuzungumzia ndicho unachzungunza bila kupindisha maana ili kwenda katika mtiririko mzuri wa maongezi na uchezaji wa nyimbo na kingine cha kuingatia ni kwa wewe ambaye tayari umesha jiandaa kimilifu unapo kuwa ONAIR yaani live kkatika matangazo hakikisha una kila kitu kilicho katika maandalizi ya kipindi cha siku na sio mbaya endapo utapata dondoo za ziada zilizo ndani ya maana ya kile unachokizingumzia.
Katika maandalizi yako hakikisha msikilizaji ni mtu mwenye nafasi kubwa sana kwakuwa ndiye mteja wao wa muhimu siku zote na kile unachokiandaa hakikisha kinamgusa kwa namna yoyote ili asichoke kukusikiliza.
5. MATUMIZI YA VIFAA VYA MATANGAZO.
Nivyema ukwa ni mzoefu au kuwa ni mtumiaji wa mara kwa mara wa vifaa unavyovitumia na kama unawakati wa kujifunza zaidi kuhusu vifaa hivyo basi usisite kufanya hivyo kwa maana unapokuwa katika matangazo hasa ya moja kwa moja(LIVE) lolote linaweza kutokea la kiufunzi na we kama mzoefu unaweza kulitatua kulingana na ujuzi ulio nao kama linaweza kutatulika hapo hapo studio.
Pia ni vema sana kijisikiliza kama wewe unajisikia vizuri kupitia headphones zako unazotumia pia kama mpangilizo(Settings) unaotumia unatoa kile usemacho au usikiacho sawa na asikiacho msikilizaji lakini kama mpangilio haukupi nafasi hiyo basi itakulazimu kuwa na kifuatilio(Monitor) inayoweza kukupa matokeo(Results) sawa na kile anachosikia msikilizaji wa mbali na eneo la matangazo ili kuleta usikivu mzuri kwa anayekusikiliza.
6. MAELEWANO NA USHIRIKIANO.
Maelewano na ushirkiano hayano maana ndefu zaidi ya mtangazaji kuwa na ukaribu na team yake anayoshirikiana nayo na hii kwa maana fupi tu ni kwamba hata kwa vipindi vya watangazaji zaidi ya mmoja mkiwa na ushirikiano na makelewana basi maongezi yenu pia yatakuwa ya kueleweka na tafsiri hii kwa msikilizaji atapenda mawasiliano yenu.
(INGAWA) Kuna wakati katika hoja ya pande mbaili au tatu tofauti itawalazimu kila mmoja wenu awe upande wake na aaandae hoja za kutetea upande aliopo ili kuleta maana kwa sikilizaji kwasababu kila msikilizaji anakuwa na mtazamo wake hivyo mnapo weka mada flani mezani msikizaji anaweza kuwa anakubaliana nayo au naapingana nayo sasa ili kupata wasilizaji wote itabidi nayi awepo anayekubali pia na anayekataa ili hapa mkitoa nafasi ya simu basi masikilizaji anaye kataa nau anayekubali kulingana na maoni yake awe mojawapo ya upande wa team yenu pale studio.
8. HISIA NA MAWAZO.
Hapa ndipo shughuli kubwa inapowa na nitatizo la wengi hasa wanaoshindwa kujizuia,mwanadamu ziku zote anakuwa na maisha ya fuaraha na wakati mwingine anaweza kuwa na kipindi cha uzuni sasa kama mtangazaji inakupasa kufanya mambo yafuatayo katika mawazo na hisia hizi mbili tofati.
(a). HISIA ZA FURAHA.
Kama mtangazaji unapokuwa na furaha kupitiliza epuka sana kuhaidi au kuzungumza jambo kupitia hisia za furaha hiyo iliyopitiliza kwasababu inaweza kusbabisha wewe kuongea jambo au kuhaidi jambo ambalo kwa mtazamo wa kawaida haliwezekani bali tu umeliongea kwa msukumo wa furaha iliyopitiliza.
(b). HISIA ZA HUZUNI/HASIRA.
Kama mtangazaji unapokuwa na huzuni au hasira inakulazimu kuziondoa katika mawazo yako ili kufanya kazi ukiwa katika hali/mood nzuri kwasababu ni rahisi wewe kujibu mtu vibaya na mara zingine unaweza kutukana kabisa ukiwa katika matangazo ya moja kwa moja(Live) na ni kosa kwa mtangazaji kufanya hivyo na kisheria unaweza kutumikia kifungo cha miaka kadhaa.
(9). KWA WASOMAJI WA HABARI.
Katika chombo cha matangazo habari ndio bidhaa kuu inayo nadiwa na watangazaji na taarifa ya habari ni jambo muhimu sana kwa wasikilizaji na hapa ndipo umakini unahitajika sana. Msomaji wa taarifa za habari unahitajika kufananya yafuatayo.
KATIKA KUIANDAA(HABARI).
Watu tumetofautiana ulimi hivyo katika usomaji kuna watu wengine maneno baadhi wao yanwawia magumu kuyasoma wakiwa huru hata wanaweza kukosea matamshi hivyo ni vyema mtu uka fanya maandalizi mapema kuweka sawa baadhi maneno yanatokupa shida katika usomaji ili uweke yake ambayo ni rahisi kwako kuyasoma bila kuteteleka bali tu yale uliyoyaweka yawe na maana sawa na yale uliyoyabadilisha.
SOMA MARA NYINGI MPAKA UIZOEE(HABARI)
Msomaji wa habari siku husika nakuwa na nafasi kubwa ya kuwasilisha kile kilichoandaliwa na sasa itakulazimu kuiweka akilini habari hiyo kwa kuisoma mpaka uozoee kiasi ambacho hata ukiwa hauna karatasi au kwa kusoma sehemu unaweza kuelezea idea nzima ya habari husika hii ni maandakizi ya kwamba jambo lolote lilitokea la kiufundi na ukasjndwa kusoma basi unaweza kuongea kutoka katika kumbu kumbu yako ya akili kwa kuwa ulikuwa nayo tayari kichwani namtazamaji asigundue tatizo lolote kutokea.
Katika kusoma unaweza kuongea neno olote ambalo halijaandikwa katika habari lakini likaleta maana na ukaendelea na habari katika maana ile ile sawa na kilichoandikwa.
9. UPOKEAJI WA SIMU NA JUMBE FUPI ZA ARAFA.
Kuwa makini sana unapokuwa ukipokea simu maana kuna wasikilizaji wengine wana chuki binafsi hivyo unaweza kupokea simu akaanza kumwaga matusi hivyo unapopokea simu kuwa tayari kukata kwa muda wowote.
Pia kwa wapigaji wa simu wastaarabu ni muhimu sana ukampatia nafasi ya kuzungumza kama ataweza kwasababu baada ya yeye kuzungumza na kujisikia pengine atakuwa shabiki mkubwa wa kituo husika kwa kuwa atajiona kuwa sehemu ya kituo kama alivyo mtangazaji kwakuwa ameogea ONAIR/HEWANI na amesikika kama mtangazaji anavyosikika kwa watu wengi.
USIPENDE kumkosoa msiikizaji kwa maana walio wengi hujisikia vibaya pindi anapokosolewa na uchukia kuwa amedharirishwa na mtangazaji jamabo amabalolinaweza kumfanya ajenge chuki kwa kituo na watangazaji wote bila kujali kuwa alitendewa hivyo na mtu wingine.
EPUKA KUKATAA.
Epuka kukataa hoja ya msikilizaji kwa maana atahisikia sawa yule aliyekosolewa na mhitiko wake utwakuwa sawa na wa yule aliyekosolewa.
UCHAGUZI WA NYIMBO ZA KUCHEZA(MUHIMU SANA).
Nyimbo zipo nyingi na zote ziko na idea tofauti hivyo ni muhimu sna kucheza wimbo kulingana na dhima ya kipindi na hoja au mada husika ili kuleta mtiririko mzuri wa kipindi na kwa mtiririko mzuru msikilizaji atapenda sana kindi husika.
Kuna wakati wa huzuni na wakati wa furaha katika jamii hivyo kama jamii impatwa na pigo babi huna budi kucheza nyimbo za huzuni ile kuedana na hali ya jamii na hakikisha hali hiyo inagusa asilimia 98% ya wasikilizaji hili kuwa sahihi kwa wote/wengi.
Pia ni vyema kusikuliza msikilizaji anapenda umchezee wimbo gani lakini ni kumhimu kuangalia kama wimbo aliochagua msikilozaji unaruhusiwa kuchezwa na kama unaendana na dhima ya kipindi hayo pia ni muhimu snaa kuyazingatia.
YAPO MENGI LAKINI HAYA N MACHACHE TU KWA LEO.
Post a Comment