Mwanzo » » KATIKA MUZIKI WA BONGO FLEVA WASANII WENYE SAUTI NZURI NA WAKALI WA CHORUS NI HAWA HAPA

KATIKA MUZIKI WA BONGO FLEVA WASANII WENYE SAUTI NZURI NA WAKALI WA CHORUS NI HAWA HAPA

Imewekwa ma Unknown siku Saturday 5 April 2014 | 21:08

Katika muziki kitu chorus ndio moyo wa muziki wenyewe,bila chorus nzuri,sidhani hata kama kuna baadhi ya nyimbo watu tungekuwa tunakaa kusikiliza,ila chorus ipate mwimbaji sasa anayeweza kuipa uhai nyimbo na kufanya ipendwe na mamilioni ya wa Tanzania.


Hii listi sasa ni baadhi tu ya wakali wanaoweza kuifanya nyimbo iwe na uhai fulani hivi na kufanya iweze ku-make headlines kwenye media mbali mbali hapa Bongo,wasanii hawa wakikaa kwenye nyimbo yeyote ile iwe ya hiphop au hata mchiriku lazima utaipenda tu kwa jinsi walivyo na vocal nzuri.


Ben pol

Muite mfalme wa chorus hapa town,asilimia 90 ya nyimbo hasa za hiphop zinazo-make headlines hapa Tzee,ujue basi kuna chorus ya Ben pol ndani yake,amebarikiwa kuwa na sauti nzuri hasa ya kuimba R&B,kuna baadhi ya nyimbo ambazo hata watu wengi ambao hawapendi muziki wa hiphop,inawabidi wasikilize tu kutokana na muunganiko mzuri kati ya r&b na hiphop,nyimbo nyingi alizowahi kufanya chorus ni;Mama ayeyoo ya Gnako,Usione hatari ya stereo,No more drama ya lord eyes na nyingine nyingi.
Ali kiba.
Ukiongelea watu wenye sauti nzuri hapa Tzee bila kumtaja Alikiba utakuwa umeingia chaka,sababu ni moja kati ya wasanii wachache wenye sauti zakufanya nyimbo yeyote iweze ku-make headlines,hata kama ni ya msanii mchanga.Japokuwa  hajatoa nyimbo yake binafsi kwa muda mrefu ,ila bado nyimbo zake nyingi kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa muziki wa bongo fleva,baadhi ya nyimbo zilizo-hit kwa ajili ya vocal lake tu ni kidela,kajiinamia za abdu kiba,nainai –ommydimpoz,na nyingine nyingi.
Jux.
Huyu ni moja ya wasanii ambao,hata kama umemshirikisha kwenye nyimbo yako  ya R&B ,unauwezekano mkubwa wa kufunikwa,na watu wakadhani bado nyimbo ni ya Jux,ni msanii asiyeshikika kwenye safu nzima ya R&B hasa kwenye upande wa chorus,anaweza kuimba chorus  tu nyimbo nzima nabado ukanunua CD yake,amefanikisha nyimbo nyingi kuweza ku-make headlines hapa bongo,nyimbo ikiwemo,Nitafanya ya kamikaze,alisema ya stamina,usiende mbali ya MRap.
Diamond Platnum.
Unaweza kusema,huyu ndio ana-run Dsm kwa sasa,na haatarajii muda wake wakukaa madarakani katika kuongoza industry ya muziki wa bongo fleva kuisha muda wowote wa hivi karibuni,kutokana na kuzidi kufanya vizuri kwenye game,nakuzidi kukubalika siku hadi siku,kama ukishakubalika na raisi wanchi yako ni sawa tu umekubalika na kila mtu.Muziki wake ndio unaofanya vizuri hivi sasa na kufanya Bongo Fleva izidi kutambulika nje ya nchi,ukingelea upande wa vocal za chorus hakuna nyimbo aliyowahi kushirikishwa ikashindwa ku-hit hadi hivi sasa.
Barnaba.

Kati ya wasani wachache sana hapa Bongo wenye uwezo mkubwa wa kuimba live,kwa gitaa tu na sauti yake nabado watu waka-enjoy,anajulikana maarufu kama Barnaba Classic,sababu muziki wake anaofanya ni classic ,yeye mwenyewe ndiye anaye uwezo wakufanya kama yeye hapa Tanzania,ni msanii ambaye hajawahi kufanya nyimbo isi-make headine katika historia ya muziki,ukiachia mbali zile ambazo amesimamia chorus,baadhi ya nyimbo ni Love me ya izzo buzness,nasema nawe ya Beka.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa