Mwanzo » » WATU MAARUFU DUNIANI WABEBA MABANGO KUPINGA UTEKWAJI WA MABINTI HUKO NIGERIA,JOHN LEGEND AWAPIGA DONGO BOKO HARAM.

WATU MAARUFU DUNIANI WABEBA MABANGO KUPINGA UTEKWAJI WA MABINTI HUKO NIGERIA,JOHN LEGEND AWAPIGA DONGO BOKO HARAM.

Imewekwa ma Unknown siku Saturday 10 May 2014 | 10:40

Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram cha Nigeria kimeendelea kuwashikilia wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na kikundi hicho katika kipindi cha wiki tatu zilizopita huku raia wa Nigeria wakifanya maandamano kushinikiza serikali kuongeza juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa wasichana hao.



Raia hao wa Nigeria wameanzisha kampeni iliyopewa jina la la Warudisheni Wasichana Wetu ‘Bring Back our Girls’ na imeungwa mkono na serikali za nchi nyingi kubwa duniani ikiwa ni pamoja na China Canada, Uingereza na Marekani huku rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akiahidi kuwa serikali yake itawasaka popote walipo na itawaokoa.

Watu mbalimbali maarufu duniani wameungana na kampeni hiyo katika mitandao ya kijamii na kupost picha wakiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Bring Back Our Girs’.

Malkia wa talk Show Oprah Winfrey, Michelle Obama, Kim Kardashian, Puff Daddy na John Legend pia ni miongoni mwa watu hao, huku Tanzania pia ikiwakilishwa na watu mbalimbali.

Puff Daddy yeye ameongeza msisitizo kwenye bango lake kwa kuandika “Bring Back Our Girls ‘Now”. Bango la John Legend yeye amewatupia dongo Boko Haram waliodai kuwa watawauza wasichana hao, “Real Men Don’t Buy Girls..”

Polisi nchini Nigeria wametangaza donge nono kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia upatikanaji wa wasichana hao.

Kundi la Boko Haram limedai kuwa linawashikilia wasichana hao kama sehemu ya kampeni yao ya kupinga elimu ya magharibi na linawataka wasichana wanafikisha umri wa utu uzima waolewe na waachane na kile wanachokiita elimu ya magharibi.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa