ALIKUWA DOGO JANJA NA SASA NI JANJARO |
Kwa kawaida msanii anapotoka na kuhit
sana huombwa kushirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wenzake nyingi na tumekuwa
tukiona baadhi ya wasanii wakidiriki kusema wamesitisha kufanya collabo na
wasanii ama wanahitaji kulipwa kiasi flani cha pesa na anaetaka kuwashirikisha.
Hii ni tofauti kwa mkali wa michano
yenye style yenye ladha ya Kaskazini Janjaro, ambae pamoja na kuwa na hits
nyingi hewani na kupiga show hadi Afrika Kusini, ameshawahi kushirikishwa
kwenye wimbo mmoja tu tangu aanze muziki, I mean tangu akiwa Arusha wakati
hajaingia kwenye mkondo mkubwa wa Muziki TZ (Main stream).
“Nilishawahi kushirikishwa kwenye
wimbo mmoja tu unaoitwa ‘Shikamoo Mwalimu’, nilifanya na Easy Muchwa,
ma-producer walioufanya ni P-Funk Majani na Chizan Brain, ile ya Madee
(Nisikilize) nilifanya intro tu na sikuandikwa kama nimeshirikishwa. Nilipokuwa
Arusha nilifanya nyimbo zangu tu lakini sikushirikishwa.” Janjaro ameiambia
tovuti ya Times Fm.
Wimbo aliofanya na
Asley(Nimeshamaliza) ulikuwa wimbo wao wa pamoja. Janjaro ameshawashirikisha wasanii
kadhaa kwenye project zake akiwemo Tunda Man, Chege, Godzilla, PNC, Jambo
Squared na wengine.
Hata hivyo Janjaro atakuwa kwenye
Project kubwa ya Dj Choka itakayowashirikisha wasanii wenye umri mdogo, na
waliotajwa kushiriki ni pamoja na Young Dee, Country Boy na M-Rap. Project hiyo
inafanyika katika studio za BHitz chini ya producer Pancho.
Huu ndio wimbo pekee aliowahi
kushirikishwa officially Janjaro:
CHANZO: TIMES FM SITE.
Post a Comment