Mwanzo » » KALA JEREMIAH ATOBOA SIRI,MAMBO YAKO HIVI....SOMA HAPA.

KALA JEREMIAH ATOBOA SIRI,MAMBO YAKO HIVI....SOMA HAPA.

Imewekwa ma Unknown siku Friday 22 November 2013 | 09:59

KALA JEREMIAH
Msanii bora wa Hip Hop kwa mwaka 2013, Kala Jeremiah ameweka hadharani kisa cha kusikitisha sana kuhusiana na maisha ya utoto wake na kusema kuwa, wakati alipokuwa mtoto mchanga kabisa, aliibiwa na watu wasiofahamika ambao walichukua jukumu la kumlea kwa miaka kadhaa kabla ya kukutana tena na mzazi wake pamoja na ndugu zake wengine.

Kala ambaye hakutaka kuzungumzia kisa hiki kwa undani zaidi amesema kuwa alipofikia umri wa miaka 16 ndipo alipokutana na mama yake mzazi, na kila anapokumbuka kisa hiki kinamfanya afikirie mambo mengi sana ambayo yanamuumiza.

Hata hivyo, msanii huyu ameahidi kuwa siku nyingine atakapokuwa sawa atajitahidi kuelezea wapenzi wa kazi zake kuhusiana na mchongo huu mzima wa kusikitisha na kusisimua kuhusiana na maisha yake ya zamani
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa