TABU LEY ROCHEREAU |
Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa hospitali kwa muda mrefu nchini Ubelgiji.
Akithibisha taarifa za kifo cha baba yake kupitia radio Okapi, mwanae Charles Tabu amesema mwanamuziki huyo aliyekuwa na umri wa miaka 73 amefariki kutokana maradhi ya kisukari na kiharusi.
Naye mwanamuziki mwenzake mkongwe Nyboma Mwandido, ameeleza kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo tangu mwaka 2008 na kumfanya ashindwe kusimama hadi mauti yalipomkuta leo asubuhi.
Tabu Ley ni mwanamuziki ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini Congo ikiwa ni pamoja na kuwa kuteuliwa kuwa mbunge na Rais Raulent Kabila, lakini pia aliwahi kuwa waziri wa Rais Raulent Kabila mwaka 1997.
Alizaliwa November 13, 1940 na safari yake ya muziki ilianza rasmi mwaka 1954 aliporekodi wimbo wake wa kwanza ulioitwa ‘Bessama Muchacha’ akiwa na African Jazz.
Katika kipindi cha uhai wake ameweza kuwa moja kati ya wanamuziki wa Rhumba waliokubalika zaidi duniani na hususani barani Afrika.
Apumzike kwa Amani.
Post a Comment