Mwanzo » » TIDDY HOTTER: UWEZO WANGU UMEMSAFIRISHA ''MICHAEL ROSS'' TOKA UGANDA MPAKA ''ONE LOVE FX''

TIDDY HOTTER: UWEZO WANGU UMEMSAFIRISHA ''MICHAEL ROSS'' TOKA UGANDA MPAKA ''ONE LOVE FX''

Imewekwa ma Unknown siku Monday 25 November 2013 | 00:24

TIDDY HOTTER

Mtayarishaji Tiddy Hotter anayemiliki studio yenye maskani yake jijini Mwanza inayokwenda kwa jina ONE LOVE FX ambayo kwa sasa ni kampuni iliyojizatiti kikazi kiasi ambacho mbali na uzalisahji wa audio pia ni kampuni inayojihusisha na uzalishaji wa video zilizo na ubora unaohitajika katika industry ya muziki wa kizazi kipya,Tiddy ameyasema hayo alipokuwa akizunumza na meza yetu ya habari ambapo amuelezea kwa undani suala la mtayarishaji anapokutana na msanii aliyendika mashairi yaliyo na sura ya bifu ndani yake sio tatizo kwa matayarishaji na game zima kwa ujumla na ameweka wazi kuwa hali kama hiyo ni moja ya challenge katika game na ni katika kurekebisha kama misingi ya sanaa inavyosema kuwa mbali na kuburudisha pia kurekebisha ni sehemu kubwa ya sanaa.
BAADHI YA VIFAA VYA KAZI ''ONE LOVE FX''
UKIKUTANA NA LOGO HII FAHAMU KUWA NI LOGO YA KAZI TOKA ONE LOVE FX

Tiddy Hotter akizunumzia msemo wa biashara ni matangazo kwa upande wake amesema kuwa hakatai msemo huo na anachoamini kwake ni kuwa kinachotangaza biashara siku zote ni ubora wa bidhaa kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuitangaza biashara yako na wateja wakafika kununua lakini wakifika na kukuta bidhaa mbovu matangazo yako yataeuka hasara,hivyo ni bora mtu ukafanya kazi nzuri hiyo ndio njia pekee ya kuitanagaza biashara yako na itadumu muda mrefu.
TIDDY HOTTER NA MICHAEL ROSS AMESAHUNANISHA VIPAJI VYAO KWA PAMOJA
Aliongeza kusema kuwa ubora wa bidhaa kuitanagaza biashara aliitaja ngoma ambayo alimtengenezea msanii toka Morogoro anayefamika kwa wengi kama Belle 9 na kusema hiyo ngoma imemleta msanii mahiri toka nchini Uganda anayejulikana kama MICHAEL ROSS ambaye ni msanii anayeiwakilisha vizuri Uganda kwa uwezo mkubwa alionao ambaye alifunga safari  mpaka ONE LOVE FX baada ya kuisikia LISTEN  ilimsukuma mpaka akafika kuonana na Producer Tiddy Hotter na mwisho ikafanyika ngoma na msanii huyo(MICHAEL ROSS na hivi karibuni ngoma hiyo itaachiwa hivyo mashabiki wakae tayari kuipokea kazi toka kwa Michael Ross aliyotayarisha TIDDY HOTTER.


Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa