SELEMEN MSINDI ''AFANDE SELE'' |
Akizungumza jana na Tanzania Daima, Afande Sele alisema kuwa filamu hiyo itazungumzia maisha halisi ya Kitanzania.
Alisema ameamua kujikita katika uigizaji wa filamu kutokana na filamu nyingi za sasa kutokuwa na maadili halisi ya Kitanzania, hivyo anataka kuonyesha njia.
“Mimi nikiangalia filamu za hao wanaojiita ma-superstar, sifiki mwisho na sijawahi kuangalia filamu yoyote ya kibongo hadi mwisho, zinaboa na unaona hakuna uhalisia wa jambo husika, watu wanaiga Wanigeria mwanzo-mwisho, wanakera,” alisema.
Afande Sele alisema kuwa ujio wa ‘Filamu Yangu’ utakuwa wa tofauti kuanzia picha, maadili na namna wasanii wake watakavyoigiza.
Aliwataka Watanzania kukaa mkao wa kula kwani filamu hiyo ipo jikoni ikipikwa kwa ustadi mkubwa.
Post a Comment