Mwanzo » » KAZI ZA SANAA ZINAINGIZA MAPATO YA TAIFA KULIKO HATA SEKTA YA MADINI.

KAZI ZA SANAA ZINAINGIZA MAPATO YA TAIFA KULIKO HATA SEKTA YA MADINI.

Imewekwa ma Unknown siku Friday, 28 February 2014 | 14:05


Msanii anayewakilisha weusi ndugu wa Rapper Joe Makini hapa anayezungumziwa ni Nikki wa Pili amebainisha kuwa kwa mujibu wa tafiti kuhusu mapato yanayoingizwa katika mapato ya taifa imeonekana kuwa industry ya sanaa kwa ujumla ndio sanaa inayoingiza pato kuliko sekta ya madini kwa kuwa ni asilimia 5 ya pato la taifa inayoingia na ukilinganisha na pato la taifa linaopatikana katika sekta ya madini na nishati ni asilimia 2 tu.


Nikki na wasanii wengine wameshiriki kutetea katiba iweke utaratibu wa kutambua kazi zinazotokana na ubunifu ikiwa ninamaanishwa kazi zote za sanaa na mpaka sasa wamerecord wimbo wa uhamasishaji na wimbo huo uko katika utaratibu wa kushootiwa video.

Hivyo kaeni tayari kwa ujio huo wa wimbo ambao unahamasisha sanaa itambulike kikatiba na mengine mengi mazuri yatakuja tuka kwa team hiyo kwakuwa wanaharakati wengi kama Kala Pina,Joe Makini,Bonta na wengine wengi wako katika utetezi na makamba yuko katika kuwaunga mkono kwa asilimia kubwa.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa