Mwanzo » » KUVAA KIMINI MTAANI NI KOSA LA KUTUMIKIA KIFUNGO JELA CHA MIAKA 10

KUVAA KIMINI MTAANI NI KOSA LA KUTUMIKIA KIFUNGO JELA CHA MIAKA 10

Imewekwa ma Unknown siku Wednesday, 19 February 2014 | 15:49


Rais wa Nchi ya Uganda Mh. Yoweri Mseven amehahalisha mswaada wa sheria wa endapo utakuwa ndani ya  vazi lenye sura ya nusu uchi,uchi kabisa au  kupatikana katika picha zenye wasifu wa ngono kuwa sheria baada ya kusaini mswaada huo kuwa sheria na adhabu kuwekwa kuwa ni kifungo cha miaka kumi jela.

Ndani ya sheria hiyo iliyowekwa rasmi nchini humo pia inazuia uvaaji wa wa nguo zinazoonesha matiti na vifua kwa wanawake kwani tabia hiyo imekithiri na uvaaji wa nguo fupi alimaarufu kama mini skirt na pia endapo utaonekana ukiwa ndani ya  nguo inayoonesha maungo ya ndani pia sheria ya nchi hiyo inakuhusu kwamadai ya kuwa uvaaji wa nguo wa namna hiyo ni uchochezi wa ngono.

Sheria hiyo iliyopitishwa imeruhusu mtu kuvaa vazi fupi katika mafunzo maalum au katika hafla za kimataifa na nguo hizo ziwe ni kwa matumizi katika eneo husika la tukio na baada ya hapo hazitaruhusiwa kwani baada ya hapo mtu atakaye endelea kuvaa hivyo atakuwa akienda kinyume cha sheria.

Pia mbali na watu wazima kuvaa uchi kuchuuliwa sheria lakini pia kwa yeyote atakaye husika kufanyisha watoto biashara ya ngono pia sheria itakuwa inamuingiza katika hatia ya kosa ambalo atastahiki kutumikia kifungo cha miaka 15 endapo shria itabaini kosa dhidi yake.


Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa