Rapper Kanye West anaendelea kufikiria jinsi ya kuwa mwanaume aliyempa zawadi ya pekee Kim Kardashian baada ya kufunga ndoa.
Chanzo kimeliambia Daily Star kuwa rapper huyo ambaye anamiliki migahawa kadhaa Chicago kupitia kampuni yake ya KW Foods LLC, amepanga kumnunulia Kim Kardashian migahawa 10 yenye hadhi za kimataifa ya kuuza vyakula kama vile hamburger.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kanye amepanga kumnunulia migahawa hiyo kutoka kwenye kampuni ya kimataifa ya Burger King Worldwide Inc na itakuwa katika bara la ulaya katika nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, ufaransa na Italia na hivyo kumfanya awe mfanyabiashara wa kimataifa.
Kanye West na Kim Kardashian wanatarajia kufunga ndoa May 24, mwaka huu jijini Paris, Ufaransa.
Post a Comment