Mwanzo » » LADY JAYDEE: MIMI NA MME WANGU KWASASA TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA.

LADY JAYDEE: MIMI NA MME WANGU KWASASA TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA.

Imewekwa ma Unknown siku Monday 31 March 2014 | 11:25

Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .

 Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?



 Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua ya kuishi katika staili hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.
 “Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.
 Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.
 “Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.


Bongoclan.com
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa