Mwanzo » » NDEGE NYINGINE YA MALAYSIA YATUA JIJINI HONG KONG BAADA YA KUPATA HITILAFU YA UMEME.

NDEGE NYINGINE YA MALAYSIA YATUA JIJINI HONG KONG BAADA YA KUPATA HITILAFU YA UMEME.

Imewekwa ma Click BongoTz siku Monday 24 March 2014 | 21:51


Wakati bado juhudi zinaendelea bila mafanikio za kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines aina ya Boeing 777-200 iliyopotea March 8 mwaka huu ikiwa na abiria 239, ndege nyingine ya shirika hilo imelazimika kutua Hong Kong, china kwa dharula baada ya hitilafu za umeme kujitokeza ikiwa safarini.Maafisa wa shirika hilo wameiambia CNN mapema leo kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A330-300 iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur kuelekea Incheon, Korea Kusini ililazimika kubadili njia na kwenda kutua kwa dharula Hong Kong baada ya wafanyakazi wa ndege hiyo kugundua hitilafu katika genereta inayozalisha umeme wa kawaida wa ndege hiyo.Kuala Lumpur ndio uwanja wa ndege ilipotokea ndege ya shirika hilo iliyopotea ambayo hadi sasa bado haijaonekanekana.Hata hivyo maafisa hao wameongeza kuwa pamoja na hitilafu iliyojitokeza lakini umeme uliendelea kuzalishwa kupitia power unit ndogo ya ndege hiyo.SOURCE: MAIL ONLINE

Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa