Mwanzo » » WEUSI WAWATUPIA ''RABBIT'' & COLLO GERE REMIX, ''NAZIZI'' NAYE ATACHAA NAO KATIKA NGOMA MOJA.

WEUSI WAWATUPIA ''RABBIT'' & COLLO GERE REMIX, ''NAZIZI'' NAYE ATACHAA NAO KATIKA NGOMA MOJA.

Imewekwa ma Unknown siku Saturday 29 March 2014 | 00:18



Ukizungumzia Weusi unazungumzia Kampuni inayojihusisha na muziki wa kizazi kipya na mambo mengine yanayotazamwa zaidi katika burudani ambapo mpaka kuikamilisha group hiyo ni muunganiko wa watu watano ingawa hivi Karibuni Kampuni hiyo kuipitia msemaji wake imemtaja Lord Eyez kama msanii aliyesimamishwa kwa muda ingawa hawakutaka kuziweka wazi sababu za wao kama kampuni kuchukua uhamuzi huo lakini ilikuwa ni uhamuzi uliochukuliwa masaa yasiozidi 48 toka kusambaa kwa taarifa za Lord Eyez kutuhumiwa kwa kesi ya wizi wa Laptop na hiyo kwasasa tunaweza sema Weusi ni watu wa nne kwasasa.


Kwasasa team ya weusi iko nchini Kenya ambapo ni katika kujipanua na kukuza muziki wao kimataifa ikiwa kwa mtazamo na hatua za haraka haraka wameonekana kujipanga vizuri kwa mwaka huu wa 2014 na kupitia video yao ya ''NJE YA BOX'' wameweza kupata kuchezwa katika vituo vikubwa vya Tv kikiwemo kituo cha Channel O zaidi kinachoendelea huko nchini Kenya ni maandalizi ya ngoma ya ''Gere'' ikiwa kama Remix na walioshirikishwa katika remix hiyo ni wkali wa hip hop kwa nchini Kenya ''Collo'' na ''Rabbit Kaka Sungura'' na zidi ya mkwaju huo ambao unatazamiwa kuwa mkali pia kuna mkakati wa kufanya kazi ya kushirikiana na mwanadada ''NAZIZI'' na mpaka sasa mambo yannelekea kuiva hivyo wadau wa muziki wa wasanii wa Weusi yaani G-Nako,Nikki wa Pili,Bonta na Joh Makini soon watashuka na mikwaju ya Dunia.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa