|
LADY JAY DEE |
Baada ya kumake more fans waendelee kumuamini kama msanii mkali wa kike toka Bongo huyu ni wakuitwa JUDITH WAMBURA a.k.a LADY JAY DEE na wimbo wake unaozungumzia maisha ya wale wajanja wajanja town wasio na muelekeo yaani kwa ufupi maisha yao ni maigizo tu lakini nyuma ya pazia hali tete kwa kuwapa jina la 'YAHAYA' katika wimbo ambao ulikuwa chini ya utayarishaji wa MAN WALTER sasa ameamua kuleta uhalisia wa 'YAHAYA' katika movie ambapo staring mwenyewe ni KULWA KIKUMBA a.k.a DUDE hivyo wadau kaa mkao wa kuisubiria bongela movie kwa jina 'YAHAYA'.
|
KULWA KIKUMBA |
Akielezea hatua ya kuelekea kufanikisha muvie hii yenye mtazamo wa kuwa kali katika tasnia ya movie bongo KULWA KIKUMBA a.k.a DUDE alisema kuwa mwanzo walifikiri iwe idea ya burudani ya muzii tu lakini mwisho wakapata idea ya kuwa wapo wapenzi hivyo ili ujumbe ufike zaidi kwa wapenzi wa burudani sekta zote wakaamua waandae muvie na hii ni kutaka tu ujumbe ufike.
Post a Comment