Mwanzo » » MWANAMUZIKI WA BEND YA FM ACADENIA AUWAWA CHINA CHANZO NI MADAWA YA KULEVYA

MWANAMUZIKI WA BEND YA FM ACADENIA AUWAWA CHINA CHANZO NI MADAWA YA KULEVYA

Imewekwa ma Unknown siku Friday 22 November 2013 | 00:17

TUANOMBA RADHI KWA PICHA YA MWILI HUU
Mwanamziki aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam, Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa na utata mkubwa. 

Kwa mujibu wa chanzo  makini kilichopo nchini China, rapa huyo alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact, Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu.

“Tulijua kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla juzi (Ijumaa) tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake kimesababishwa na nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua na moto au mtu aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho.

Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu aliwasiliana  na Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za Haristot.

Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa.

“Haristot alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa