Young Killer Msodoki |
Young Killer alipokuwa akihojiwa katika interviews zake toufauti na vyombo vya habari alikuwa akihaidi kurudi shule na kuweka wazi kuwa mbali na yeye kujikita katika muziki zaidi lakini bado katika maisha yake shule ina nafasi kubwa sana.
Katikati mwa mwaka jana Young Killer aliwataka wadau wamsupport ili aweze kurudi darasani jambo ambalo baadae lilipigiwa kimya na mwisho juma liliopita ameweza kujiunga katika chuo cha ''Green Pasture'' ambapo anachukua msomo ya ''Information Technology(IT)'' na leo kupitia account zake mtandao ya kijamii amepost picha inayomuonesha akiwa darasani yenye ujumbe ''am...back...class'' makini masomoni huku akiwa na headphone shingoni jambo linaloashiria kuwa mbali na kurudi masomoni lakini bado yuko karibu na muziki.
Hongera kwake na hili liwe somo kwa wasanii wengine ambao wameshajitoa katika suala la shule kuwa elimu haina mwisho hivyo wanawezakujiendeleza kama anavyofanya Young Killer kwasasa.
Post a Comment