Mwanzo » » APPLICATION YA WHATSAPP KUNUNULIWA NA MMILIKI WA FACEBOOK.

APPLICATION YA WHATSAPP KUNUNULIWA NA MMILIKI WA FACEBOOK.

Imewekwa ma Unknown siku Thursday, 20 February 2014 | 22:25



MARK ZUCKERBERG
Miliki wa mtandao wa mawasiliano wa Facebook Mark Zurkerberg  ameingia katika makubaliano na mmilikiwa WhatsApp kuinunua application yake ya WhatsApp iliyoanzishwa mnamo mwaka 2009 na wamarekani(C.E.Os) Brian Acton na mwenzake Jan Koum kwa pesa za Kimarekani Dolla Billion 16 na hisa na hakutakuwa na mabadiliko yoyote na itabaki ikijitegemea kama alivyofanya aliponunua Application ya Instagram ambapo hata hiyo aliiacha ikaendelea kufanya kwa kujitegemea.

Jan Koum

JAN KOUM                                                             NA                                         BRIAN ATON


Makubaliano ya kununua Application hii ya WhatsApp kwa Mmiliki wa Facebook ni asilimia 11 tu ya soko la Facebook Duniani kote  na pia Facebook bado ni Kampuni kubwa hata kushinda ile ya Google walipionunua  Motorola Mobility ambapo hiyo waliinunua kwa Dollar Billion 12.5 za Kimarekani na kampuni ya Microsoft walipoinunua Application ya Skype kwa Shilling Billion 8.5 za Kimarekani.



Kimatumizi duniani kote Application ya WhatsApp inawatumiaji zaidi ya mtandao kama twitter ambapo WhatsApp inawatumiaji Million 450 ambapo mtandao wa Twitter iko na watumiaji 241 jambo ambalo inaonesha kupisha sana kwakuwa mtandao wa twitter unaweza kutumika kwa kifaa chochote chenye uwezo wa internet tofauti na WhatsApp kwasababu WhatsApp inatmika kwa vifaa pekee venye uwezo wa Internet na kusupport Application hiyo ya WhatsApp.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa