Mwanzo » » SASA MAPENZI YA JINSIA MOJA UGANDA NI KOSA KUBWA UNALOWEZA KUFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA.

SASA MAPENZI YA JINSIA MOJA UGANDA NI KOSA KUBWA UNALOWEZA KUFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA.

Imewekwa ma Unknown siku Monday, 24 February 2014 | 16:22

Rais Yoweri Mseveni(Uganda)
Nchini Uganda Rais Yoweri Mseveni katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake mbele ya maafisa wakuu wa serikali na waandishi wa habari wa vituo tofauti ametiasaini mswaada kuwa sheria wa kutumikia adhabu kali kifungo cha kwenda jela kwa watu watahusuka na vitendo vya mahusiano ya jinsia moja.

ALAMA ZA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA



Baada ya mswaada huo kitiwa saini na Rais Mseveni basi watakao bainika kushiriki vitendo vya jinsia moja watatumikia kifungo cha miaka 14 jela kama watenda kosa wataonekana kuwa ni kosa lao la kwanza kubainika na wale watakaobainika kubainika na kosa la namna hiyo kwa mara ya pili au zaidi basi wataumikia kifungo cha maisha jela hata kama washiriki wa mapenzi hayo watakuwa wamekubaliana kufanya hivyo.

HII NI BENDERA INAYOMAANISHA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA


Hata hivyo kundi lingine la watu watakaokumbana na makali ya sheria hiyo ni pamoja na watakaobainika kuhusisha watoto katika mapenzi ya namna hiyo na walemavu wa viungo na akili pia kuhusika kwa namna yoyote uambukizaji wa virusi vya ukimwi kwa kundi hilo tajwa.

Mswaada wa sheria hiyo kusainiwa na Rais wa Uganda emeleta hisia tofauti ambapo Mashirika ya kimataifa ya utetezi wa haki za binadamu yamelaani uhamuzi huo na Mwanume anyejulikana kama Moses toka nchini Uganda ambaye anashiriki mapenzi ya jinsia moja amelazimika kutafuta hifadhi nchini Marekani kuikimbia sheria hiyo ambayo moja kwa moja haimruhusu kufanya hivyo.

MOSES

Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa