Mwanzo » » TAASISI YA KIISLAMU YAITAKA YOUTUBE KUONDOA VIDEO YA WIMBO WA KATY PERRY.

TAASISI YA KIISLAMU YAITAKA YOUTUBE KUONDOA VIDEO YA WIMBO WA KATY PERRY.

Imewekwa ma Unknown siku Wednesday 26 February 2014 | 10:59

Video ya wimbo wa msanii wa kimataifa Katy Perry Ft. Juicy J unaokwenda kwa jina Dark Horse imeandikiwa ''Petition'' na taasisi ya kiislamu ya Uingereza inayojuliakana kama Shazad Iqbal kwasababu baada ya wao kuitazama imaonekana ikimkashfu mungu  na kuipa ushindi nguvu za giza.

Katika dakika 1 na Dakika 15 ya video ya wimbo huo inaonekana mtu aliyevaa kufu wenye maandishi ''Allah'' kwa maana ya mungu na kushindwa kuishinda nguvu za giza na kuungua jambo ambalo linaonekana ni kumkosea mungu heshima na maneno ya ''so you wanna play with magic'' ndio yanayosikika kuonesha kuwa mungu anakosa nafasi na kushujudiwa nguvu za giza.


Taasisi hiyo ya kiislamu baada ya kuandika 'Petition'' kwa kampuni ya Youtube ombi hilo mpaka sasa limeshapata 40,000 kuunga mkono kuwa Video hiyo itolewe na inatazamiwa kuwa kama zitapatiakana saini 100,000 basi video hiyo itaondolewa.


Video hiyo ya Dark Horse imeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya Billbord top 100 kwa week nne mtawalia na hiyo ngoma inapatikana katika Albumya Katy Perry inakwenda kwa jina ''Prism'' na zipo ngoma nyingine ambazo hatujajua kama zinaweza kuwa na dhima kama zinazopatikana katika hii ya Dark Horse.


Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa