Mwanzo » » TCRA YAFUNGIA VIDEO ZA WASANII ZINAZOKIUKA MAADILI YA KITANZANIA,DULLY,JUX NA SNURA WAKUMBWA.

TCRA YAFUNGIA VIDEO ZA WASANII ZINAZOKIUKA MAADILI YA KITANZANIA,DULLY,JUX NA SNURA WAKUMBWA.

Imewekwa ma Unknown siku Thursday, 20 February 2014 | 17:48

DULLY
Serikali ya jahumuri wa Tanzania kupitia mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imefungia video za baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya kwa kosa la kukiuka maadali ya kitanzania ikiwa ukiukaji wa maadili ni kile kinachooneshwa katika video hizo jambo ambalo ni pamoja na uvaaji vibaya wa watoto wa kike pamoja na maneno yenye wasifu wa matusi katika video za wasanii hwao waliofungiwa.

JUMA JUX


Orodha ya video za wasanii wa Tanzania wanaofanya muziki wa Bongo Fleva ni pamoja na video ya wimbo wa Brothermen Prince Dully Sykes,Juma Jux na Snura. Video ya Prince Dully Sykes ni ile ya Kabinti Special,na ya Juma Jux ni ile ya Uzuri wako na ile ya Snura ya wimbo wake wa Nimevurugwa.

SNURA

Vazi hili naloonekana mwandada amelivaa katika shor tofauti ni moja ya sababu za kufungiwa kwa Video ya Kabinti Special ya Dully.

Maneno yaliyoandikwa katika Tshirt hii aliyovaa Diamond Platnumz ni moja pia ya sababu zilizosababisha Video ya Kabinti Special kwa kuwa ni kama alikuwa ni tusi kwa jeshi.


Sababu ya ngoma ya Dully kufungiwa ni maneno mabaya yaliyo katika  T-shirt ya Diamond Pltnumz na Video Queen aliyokuwa kajitupia katika kijivazi cha kuogelea ambapi anaonekana katika muonekano wa nusu uchi na ile ya Jum Jux yaani hapa naizungumzia Uzuri wako na pamoja na Video Queen anayeonaka humo kuwa katika movement za malavidavi na Juma Jux kitandani ikiwa Jux kavaa Suruali na Boxer nje nje na hii nyngine ya Snura mamaa wa Mjanga ni uvaaji na mauno yanayotembezwa mle ndani ingawa kama iveo hizo zitarekebishwa na zikapita katika team ya kuzikagua basi zinaweza kuendelea kuoata airtime katika vituo vya television.


KABINTI SPECIAL VIDEO-DULLY






UZURU WAKO VIDEO -JUX






NIMEVURUGWA VIDEO-SNURA MUSHI





MTAZMAO KUHUSU HILI.

Nikweli kuwa wasanii wa sasa hivi wanapigania soko la kimataifa,kujizolea mashabiki pamoja na kutendea mashabiki haki kwa video kali ila tu naweza kutoa angalizo kwa waelekzaji(Video directors) kuwa kila jambo wanalolipanga lionekane katika video ya msanii kuna kila sababu ya kuliangalia kwa umakini kwasabu naamini wanafahamu vyema maadili ya kitanzania na wanaweza kujua nini kuonekane na nini kiasionekane katika video kimsingi.

Kama idea hizi za watoto wa kike kuvaa vibaya ni idea za wasanii basi watakuwa wanpoteza maana ya kuwa wao ni vioo vya jamii kwasababu hii hali imefikia hatua ya kuwa kuna video za kibongo zinzoweza kuchezwa katika television mfululizo na kama uko na wazazi ngumu kwako kundelea kuzitazama kwakuwa siku hizi idea za nusu uchi zimetwala video za wasanii wa kitazania na na kwa wale wanaochipukia hili ni darasa kwako ili wasije kuingia katika janga la kufungiwa na wao kama walivyofungiwa wasanii hawa.

Hivyo basi hilo linaweza kusaidia lakini pia na wasanii wenyewe mna uhuru wa kukataa jambo linalowekwa katika video yako kwasababu endapo hauta kagua kazi yako ili isikuingize matatani unaweza kuingia hasara ya kazi yako mwisho wa siku ukashuka kimuziki ingagwa wapo baadhi ya wasanii wanakili kuwa vile ambavyo vina sababisha video kupigwa marufuku kwa Tazania ndio vinaongeza views katika chanel ya YouTube jamba ambalo naweza kukubali na wakati mwingine nikakataa kwasababu mbona video za msanii kama Diamond Platnumz ziko na Vies kibao na hazjafungiwa?.


Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa