Mwanzo » » MLINZI WA RAIS BARACK OBAMA AFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUPIGA TUNGI KAZINI.

MLINZI WA RAIS BARACK OBAMA AFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUPIGA TUNGI KAZINI.

Imewekwa ma Unknown siku Wednesday 26 March 2014 | 23:34


Jarida la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba askari watatu ambao ni walinzi wa president wameachishwa kazi kwa muda na kurudishwa nyumbani ili uchunguzi ufanyike.
Askari mmoja kati ya hao alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli moja huko Amsterdam ambapo Obama alienda kwa ajili ya mkutano wa mambo ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi kwa muda huku uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa