Mwanzo » » WOLPER KUGOMBEA PEDESHEE LA KIKONGO MARA BAADA YA KUACHANA NA MPENZI WAKE. KISA KIKO HAPA.

WOLPER KUGOMBEA PEDESHEE LA KIKONGO MARA BAADA YA KUACHANA NA MPENZI WAKE. KISA KIKO HAPA.

Imewekwa ma Click BongoTz siku Tuesday 25 March 2014 | 10:02



KUCHAMBANA, kutoleana lugha chafu ndiyo ishu iliyopo kwa sasa kati ya nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011 iliyomtoa mlimbwende Salha Israel, Husna Maulid kufuatia madai kwamba, wanamgombea mwanamume Mkongo aliyejulikana kwa jina moja la Mwami. 
“Ni kweli kabisa, Wolper amenichukulia mwanaume wangu. Mi nimemshangaa sana. Halafu eti ananitumia meseji za ajabu ajabu mimi, eti anasema hajanichukulia bali ni bwana ‘ake siku nyingi (huku akionesha meseji hizo).
Kwa mujibu wa Husna, awali siku hiyo alitaka kwenda kumfumania Wolper na Mkongo huyo kwenye hoteli waliyokuwa wakila chakula lakini machale kama yalimcheza wakaondoka.



 Kwa mujibu wa chanzo chetu, Husna ndiye aliyeanza kuwa na uhusiano na Mkongo huyo mwaka jana na kila anapofika nchini hutanua naye kwenye ‘viwanja’ mbalimbali.
 “Husna ndiye mwenye mwanaume, akija Bongo wako wote, lakini hivi karibuni ghafla tu, jamaa kaja na kuwa na Wolper, Husna kapigwa chini, sijui Wolper alimpatia wapi?” kilisema chanzo hicho.
 Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Husna na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka kwa kusema:

 
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, 'mlimbwende' Husna Maulid.

 Baadhi ya meseji hizo zinaonesha Husna akijibu mapigo upande wa pili huku akishambulia kwa maneno makali kufuatia madai kwamba anatembea na Mkongo wake.
 “Jana (Ijumaa) alikwenda naye hoteli…(anaitaja jina) iliyopo Masaki (Dar), wakala chakula kisha wakaenda kulala hoteli… (pia anaitaja jina). Mimi najua kila kitu,” alisema Husna akionesha hasira.
 Baada ya kuzungumza ana kwa ana na Husna, Uwazi lilimsaka Wolper kwa njia ya simu ili kumuuliza lakini hakupokea. Wakati mwingine simu yake ilipopigwa ilionekana kuwa bize.
 Hata hivyo, ili kumpa nafasi zaidi ya kujieleza, Wolper alitumiwa meseji saa 5:05 asubuhi ikiwa na mashitaka yote ambapo ‘ilideliva’ kwenye simu yake, lakini pia hakuijibu mpaka saa 10:13 jioni wakati gazeti hili linakwenda mitamboni.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa