Mwanzo » » WAWILI HAWA WATAIKOSA MECHI KALI KATI YA MAN U NA BAYERN ITAKAPIGWA SIKU YA KESHO.

WAWILI HAWA WATAIKOSA MECHI KALI KATI YA MAN U NA BAYERN ITAKAPIGWA SIKU YA KESHO.

Imewekwa ma Unknown siku Tuesday 8 April 2014 | 20:38

United_2869643bKlabu ya Manchester United leo mchana imesafiri kuelekea jijini Munich kwa ajili ya kupambana na Bayern Munich katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora.
Katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu hiyo jina la mshambuliaji Wayne Rooney lilikuwepo pamoja kwamba iliripotiwa anaweza asiichezee timu hiyo kesho, lakini majina ya kiungo Marouane Fellaini na mlinzi Rafael hayakuwemo katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu kwenda Munich ikielezwa kwamba wana majeruhi na hivyo hawataichezea timu hiyo.
United tayari imewasili Ujerumani na leo jioni walifanya mazoezi katika uwanja wa Allianz Arena kujiandaa na kipute cha kesho.
Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford wiki iliyopita.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa