Mwanzo » » CHECK TECKNOLOGIA ILIVYO MUUMBUA MWIZI WA SIMU MARA BAADA YA KUJARIBU KUWEKA PASSWORD MARA KADHAA BILA KUFANIKIWA.

CHECK TECKNOLOGIA ILIVYO MUUMBUA MWIZI WA SIMU MARA BAADA YA KUJARIBU KUWEKA PASSWORD MARA KADHAA BILA KUFANIKIWA.

Imewekwa ma Unknown siku Tuesday, 6 May 2014 | 20:49

Screen Shot 2014-05-06 at 1.37.32 PMJinsi teknolojia inavyokua kuna baadhi ya vitu kwenye miaka inayokuja vitashindikana kufanyika kutokana na maboresho yanayofanyika kuvidhibiti.
Unaambiwa kuna simu ya mkononi iliibwa lakini baadae kidogo ikatuma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha kuwa ndiye mmiliki wake.
BBCSwahili.com wameandika polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo aina ya HTC ambayo iliibwa kutoka kwenye koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.
Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza namba ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.
Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanaume huyu alipojaribu kuingiza namba hiyo bila kufanikiwa ambapo email ya Mwanafunzi huyo ndio ilituma ujumbe kwa polisi kuwataarifu kuhusu wizi huo.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa