Mwanzo » » BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA AJIONDOA UHAI KWA KUJIPIGA RISASI MWENYEWE.

BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA AJIONDOA UHAI KWA KUJIPIGA RISASI MWENYEWE.

Imewekwa ma Unknown siku Wednesday 2 July 2014 | 16:43

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Asa Mwambene. Mwambene amesema mpaka sasa chanzo cha kifo cha balozi huyo hakijajulikana.
Nitaarifa ya kusikitisha na ni pigo kwa Taifa la Libya lakini pia kwa Taifa la Tanzania.
Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa