 |
SHARO MILLIONEA |
Ni mwaka sasa tangu pengo la familia ndugu,jamaa,marafiki na sanaa nzima kwa ujumla kumpoteza kijana aliyekuwa anakila sababu ya kuigwa na wasanii na vijana wengine waliokuwa na vipaji katika ulimwengu huu wa changamoto...aliyetutoka mwaka mmoja sasa HUSSEIN RAMADHAN ambaye alifahamika sana kwa wengi kama SHAROMILLIONEA ambapo ilikuwa Novemba 26 mwaka 2012 mida ya usiku hivi ndipo waliowengi walipata taarifa za ajali ya gari ya msanii huyo aliokuwa safari akiendesha gari kuelekea kwao Muheza Tanga na kupelekea kifo chake.
Hivyo hatuna budi kumkumbuka kwa sala na kumuombea alazwe pema peponi AMEN.
Post a Comment