Mwanzo » » MC D WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA.

MC D WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA.

Imewekwa ma Unknown siku Tuesday, 28 January 2014 | 09:47

MC D Enzi za uhai wake.
Alikwenda kwa jina la Masoud Mohamed lakini waliowengi na wafatiliaji wa muziki wa dance walimfahamu kama MC D kama mpiga tumba ambaye kwa taarifa ni kuwa usiku wa kuamkia leo ametangazwa kufariki dunia huko Moshi katika hospitali ya KCMC Moshi na msemaji wa Band ya twanga pepeta Hassan Rehani kuthibitisha uweli wa taarifa hizo.

Wiki kadhaa MCD alikuwa ameonekana kupata nafuu ambapo kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu walikuwa wamemalizana na matibabu ya kifua kikuu kilichokuwa kikimsumbua na alikuwa amemaliza doze ya kifua kikuu.

MCD alipokuwa akiongea na watu wake wa karibu alikuwa akiwaambia kuwa kwasasa jinsi anavyojisikia mapema mwaka huu atarejea jukwaa kama kawaida na ataendelea na kazi yake na mara hii atakuwa moto wa kuotea mbali.

Enzi za uhai wake MCD amewahi kufanya kazi na band kadhaa hapa nchini Tazanania na miongoni mwa Band hizo ni pamoja na Diamond Sounds,Mshujaa Band pamoja na Twanga Pepeta.


MUNGU AILAZE ROHO YA MERHEMU MASOUD MOHAMED PEMA PEPONI,AMEN.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa