Mwanzo » » DIAMOND PLATNUMZ NA DULLY SYKES NDANI YA NGOMA MOJA.

DIAMOND PLATNUMZ NA DULLY SYKES NDANI YA NGOMA MOJA.

Imewekwa ma Unknown siku Monday, 24 February 2014 | 20:58

DULLY SYKES NA DIAMOND PLATNUMZ
Wale ni Diamond Platnumz na Dully Sykes na kwa pamoja tunatambua uwezo wa kila mmoja,Dully ni wa muda mrefu na ni msanii aliyedumu kwa muda mrefu akitoa hit baada ya hit na vivyo hivyo kwa Nasib Abdul alimaarufu kama Diamond Platnumz,tangu wakutane katika collabo la utamu ambalo pia Ommy Dimpoz alishiriki walikuwa hawajakutana tena katika audio yoyote bali tu katika video ya Dully ambapo T-Shirt aliyokuwa amevaa Diamond ilikuwa ni moja ya sababu  zilizopelekea kichupa hicho kufungiwa kwa kuwa Maandishi yaliyokuwa yameandikwa katika t-shirt hiyo hayakuwa mazuri kimaadili na wakapewa nafasi ya kufanyia marekebisho kisha kama itaonekana kuwa sawa itaruhusiwa kuchezwa katika vituo vya Television..


Kufungiwa kwa video ya Kabinti special ya Dully Sykes haikuwaweka katika kikwazo cha kushindwa kuendelea kufanya kazi kwa wawili hawa yaani Platnumz na Dully na soon wanakuja na collab la pamoja na ngoma itakwenda kwa jina ''CHIPOLOPOLO'' ikiwa ni chini ya utayarishaji wa Dully mwenyewe kama Producer katika studio za STUDIO 4.12 zinazomilikiwa na Dully pia na akitoa taarifa za kuaminika kuhusu ujio wake mpya na Diamond Dully amesema kuwa wako katika mkakati wa kutaka ngoma hiyo itakapotoka itoke na kichupa kwa pamoja na mtajwa atakayetayarisha video hiyo ni moja katika ya watayarisjai wakubwa kutoma hapa nchi ambaye amewezesha video za wasanii wa Tazania kufika level ambao ni za kimataifa na hata baadhi ya video alizokwisha wahi kuandaa kutajwa kuingia katika tuzo ADAM JUMA wa Viisual Lab(Next Level).

WADAU WA MUZIKI KAENI MKAO WA KULA.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa