Mwanzo » » LINEX SUNDAY ''MJEDA'' AWAWAKIA MAPRODUCER WANAOCHIPUKIA, NI BAADA YA NGOMA YAKE KUACHIWA BILA RUHUSA.

LINEX SUNDAY ''MJEDA'' AWAWAKIA MAPRODUCER WANAOCHIPUKIA, NI BAADA YA NGOMA YAKE KUACHIWA BILA RUHUSA.

Imewekwa ma Click BongoTz siku Friday 28 March 2014 | 07:42

LINEX LINENGA
Msanii Sunday Mjeda a.k.a Linex, amewalaumu producers wadogo wasiokuwa na majina makubwa katika game kuwa ndio wanao ongoza kwa kuvujisha ngoma za wasanii wenye majina ambao huwa wanafanya na producers hao kiroho safi.
"unajua wanachokosea wanafanya haraka,kwanza kitu ambacho wanapaswa kujua mimi siwezi ku-record wimbo siku moja, kesho ukaniambia niupeleke kwa mamilioni ya watu haiwezekani. Nikijia ku-record kwako maanake nikichukua demo naenda nyumbani kisikilizanijue wapi nafanya nini hapa naweka hivi hapa natoa ili kwenye jamii nipeleke kitu kizuri"

"kitendo cha kupeleka ule wimbo bila kuniambia amenikwaza kwasababu ule wimbo ulikuwa ni wimbo mzuri, ningepata time ya kufikiria nini niweke nini nisiweke tungepata wimbo mmoja mzuri kabisa ambao tungeweza hata kuutoa amefanya tu harakaharaka kwahiyo amenikwaza sana."

"Mwaka huu mimi sijatoa wimbo, kwahiyo ninachoomba media zisipige huo wimbo na sitakuja kuutoa maana tayari ameshanikwaza mi naandika everyday kwahiyo sitakuja kuutoa huo wimbo tena daima na milele.

Ma-producer wadogo kwa ushauri tu ni kwamba wanafeli wanapo release ngoma za watu, watasababisha wasanii wakubwa wakaendelea kufanya kazi na producers wakubwa wakati wao wanavipaji na wanauwezo wa kupiga ma-beat makali kuliko hata baadhi ya ma-producers wakubwa na wako juu, kwahiyo watasababisha tushindwe kuwafata kwasababu hawana respect na kazi za watu."
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa