Mwanzo » » MAAFA YA MVUA KUBWA YAMKUTA BABU AYUBU,AHAMA NYUMBA NA GARI LAKE LAGEUKA CHUMACHAVU.

MAAFA YA MVUA KUBWA YAMKUTA BABU AYUBU,AHAMA NYUMBA NA GARI LAKE LAGEUKA CHUMACHAVU.

Imewekwa ma Unknown siku Monday 31 March 2014 | 15:25




Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa 28 March 2014 imeleta maafa maeneo Kimara na Kuvunja Nyumba ya msanii wa Sauti na Muziki wa Kizazi Kipya maarufu kama Babu Ayubu, yeye mwenyewe anasema siku hiyo alirudi saa saba usiku na kujifungia ndani kwake lakini ilipofika mida ya saa kumi usiku akaskia kishindo Puup kushusha mguu wake kutoka kitandani akaona maji yapo kimo cha ugoko wake akajaribu kufungua mlango ukawa haufunguki kumbe ukuta ulikua umeangukia mlangoni na kuzuia usifunguke ndipo alipopiga makelele kwa majirani, wakafika na kumpa msaada lakini alipotoka nje akakuta gari lake limepondwa na matofali 1200, Babu anasema Gari hilo haliwezi tena kukaa barabarani so itabidi auze kwenye vyuma chakavu na kuhusu kulala amesema atalala katika nyumba yake nyingine kwasababu alikua amejenga nyumba tatu katika eneo moja na iliyoathirika ni moja tu.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa