Mwanzo » » MZEE WA MIAKA 100 ASEMA YUKO TAYARI KUNDELEA NA ELIMU YA SECONDAR BAADA YA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI.

MZEE WA MIAKA 100 ASEMA YUKO TAYARI KUNDELEA NA ELIMU YA SECONDAR BAADA YA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI.

Imewekwa ma Unknown siku Monday 31 March 2014 | 00:23


Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100. Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani) ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya msingi baada ya kusoma kwa mwaka mmoja tu na kurejea kuisaidia familia yake masikini kufanya kazi za nyumbani. Hata hivyo alirejea shule kuendelea na masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa na mmoja wa wajukuu zake.


Manuela Hernandez akiwa ameshikilia cheti chake cha kuhitimu elimu ya msingi. Hivi sasa tayari amekabidhiwa diploma yake ya elimu ya msingi katika sherehe iliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini. Bibi Hernandez amesema sasa ataendelea na masomo ya elimu ya sekondari. Zaidi ya nusu ya wakazi wa jimbo la Oaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15 hawajamaliza elimu ya msingi.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa