Mwanzo » » STERIO ALIMKAMATA VICTORIA KIMANI NA WAKAFANYA KAZI.

STERIO ALIMKAMATA VICTORIA KIMANI NA WAKAFANYA KAZI.

Imewekwa ma Unknown siku Monday 31 March 2014 | 21:12


Member wa zamani wa Lunduno, Stereo ni mmoja kati ya wasanii waliopata nafasi ya kufanya wimbo na Victoria Kimani wa label ya Chocolate City ya Nigeria.
Stereo ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa alifanya wimbo huo na mkali huyo toka Kenya wiki tatu zilizopita ndani ya studio za Bongo Records na producer P-Funk Majani.
Licha ya kuwa wengi walimfahamu Stereo kwa flow za hip hop anazidi kuonesha upande mwingine wa kile anchoweza kufanya.
“Nimefanya wimbo na Victoria, unaitwa Kila Kitu na altenative tittle ya huo wimbo ni I Will Never Let You Down. It’s kind of ragga/Dancehall na yenye fusion ya rap ndani yake.” Amesema Stereo.
Rapper huyo ameeleza sababu za kutaka kufanya kazi na mrembo huyo wa Kenya ambaye mixtape yake ya Queen Victoria aliyofanya Marekani ilimpa nafasi ya kukubalika zaidi na watu wengi duniani.
“Nilitaka kufanya na Victoria kwa sababu nilitokea kumuelewa sana tangu nilipoanza kusikiliza kazi zake especially mixtape yake ya kwanza ile Queen Victoria. Kwa hiyo nilijaribu kusikiliza nyimbo nyingi, kuna nyimbo kafanya na Busta Rhymes, kuna nyimbo kafanya na Jadakiss nikagundua she is talented na anasauti nzuri.
“Businesswise yuko vizuri, kibiashara yuko kamili kila angle, so hizo ni sababu ambazo zilipelekea mimi kutafuta kufanya kazi na Victoria.” Stereo alifunguka.
Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa