Mwanzo » » A.Y NA TUNDA MAN WAJITETEA KUHUSU KUSHOOT VIDEO NJE YA NCHI.

A.Y NA TUNDA MAN WAJITETEA KUHUSU KUSHOOT VIDEO NJE YA NCHI.

Imewekwa ma Unknown siku Friday, 21 February 2014 | 09:59

A.Y

Baada ya malalamiko kwa waandaaji wa video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoa malalamiko kwenda kwa wasanii kwa vitendo vyao vya kutowathamnini baada ya kufanikiwa kimuziki yaani kwa kutoa maelezo ya kuwa wasanii wanapokuwa ndo wanchipukia ufanya kazi na wao kwakuwa na bajeti ndogo lakini wakisha piga hatua kimuziki na kupata shows kadhaa uhamua kwenda nje ya nchi kushoot video badala ya kurudi kwa waandaaji wao wa tangu awali ili washoot video ya bajeti kuwa jambo linaloashiria kudharauliwa kwa waandaaji hao na kulipotezea taifa mapato kwakuwa wanapoenda nje ya nchi ulipa kodi kupitia matmizi yao wakiwa huko.

TUNDA MAN
Msanii Tunda mani naye ni miongoni mwa wasanii walioshoot video siku za hivi karibuni na yeye alijitetea kuwa kushoot video nje mtu unaweza kufanya hivyo kama utaona kuna ulazima wa msanii kufanya hivyo na kama pia msanii ataweza kumsafirisha muandaaji wa video yake afanye hivyo kwakuwa haya yeye katika video ya Msambinungwa amemsafirisha muandaaji wake katika sehemu zote alizopenda kushoot video yake katika kutafuta location nzuri na miongni mwa maeneno aliyoenda kushoot vipande vya vieo ya msambinungwa ni Nairobi,Mombasa na Jijini Dar es Salaam na kuongeza kwa kusema kuwa mbali na kuwa ukishoot nje ya nchi video yako kunaweza kukuongezea  connection lakini pia ukishootia video bongo na director mzuri na kwa Bajeti iayokidhi basi bado video inaweza kukufikisha mbali hata kuchezwa katika vituo vya tv vya kimataifa.



Ambwene Yessaya yeye pia ni moja ya wasanii waliotoka sna nje ya nchi kushoot video na yeye katika kujitetea na kutoa sababu zinazomfanya aende kushoot video zake nje ya nchi ni pamoja na waandaaji wa nje ya nchi ambao mara nyingi uwa na connections za video zao kuchezwa nje ya nchi na vituo vikubwa vya kimataifa mbali na wao kuwa waandaaji wa video zenye ubora hivyo hiyo ameotaja kama moja ya sababu zinazompelekea mara nyingi yeye kuvuka border na kushoot nje ya nchi.


MTAZAMO KUHSU HILI.

Kushoot nje ya nchi ni moja ya sababu ambazo kweli zinaweza kufikisha video ya mtu mbali lakini bado bajeti katika kuandaa video inaonekana kuwa msingi mzuri na imara wa kufanya video kali hata ukiwa hapa hapa nchini Tanzania na kama bajeti hiyo itatumiwa na muandaaji mbunifu na mwenye upeo mkubwa katikamambo ya uandaaji wa video za muziki.

MSIKILIZE TUNDA MAN HAPA

Share habari hii :

Post a Comment

WADHAMINI WA BLOG YETU

SIKILIZA CLOUDS FM ONLINE HAPA

TUFUATE HAPA

WASOMAJI WETU

FACEBOOK

DONDOO ZA MWEZI

TWITTER

BLOG ZA WADAU

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
HAKIMILIKI © 2013. CLICK BONGO TZ - Haki zote zimehifadhiwa