|
R.I.P NGWEAR
|
Miliki na Mtayarishaji katika studio za BLACK CUTAINS REC Mswaki aliyeibuka na kujulikana zaidi mara baada ya kifo cha Rapper Albert Mangwear kwa kuwa kipindi cha msiba aliachia ngoma iliyokwenda kwa jina OPEN LETTER ngoma aliyokuwa akisikia sauti ya Ngwear sauti ambayo ilikuwa ni ya kuigiza ambapo aliigiza ili kumuenzi Albert Mangwear na ilikubalika kiasi cha kupata Downloads za kutosha na hakuishia hapo alipanga kufanya makubwa kupitia sauti yake inayoigizwa vilivyo na kusound kama ya Ngwear na hivi karibuni ameachia ngoma mpya kabisa iliyokwenda kwa jina GETHO nyimbo inayoelezea maisha ya getho na kama we ni mfailiaji wa muziki wa Ngwear utakumbuka kuna ngoma ya Ngwear iliyokwenda kwa jina la GHETO LANGU na hiyo pia ilikuwa ni moja ya kumuenzi Mangwear na kutaka kuikuza project yake ameamua kutengeneza Album itakayokwenda kwa jina KEEPING NGWEAR ALIVE na kuendelea kutumia Style ya Albert Mangwear Mswaki ameamua siku ya kesho kufunga safari kwenda Morogoro iliko familia ya Ngwear kwa ajili ya kupata Baraka na ruhusa ya matumizi ya sautikatika project zake.
Post a Comment