Basi la magereza lililokuwa limebeba mahabusu na wafungwa likisindikizwa na askari polisi limeshambuliwa kwa risasi na watu wenye silaha wanaosadikika kuwa ni majambazi, ameeleza shuhuda mmoja.
Watu hao wenye silaha walikuwa wakitokea kwenye kituo cha Nyerere jijini Dar es Salaam walilishambulia basi hilo na kuwajeruhi baadh ya askari.
Mahabusu waliokuwa kwenye basi hilo walianza kushangilia wakati tukio hilo likifanyika, huku ikisemekana kuwa lengo la shambulio hilo ni kuwatorosha mahabusu hao.
Taarifa zinasema kwamba baada ya kushambulia basi hilo, majambazi hao waliweza kukimbia mahali pasipojulikana.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka jeshi la polisi na jeshi la magereza kuhusiana na tukio hilo la leo.
Post a Comment